The donee could no longer lawfully draft, sign or verify anylegal or thereafter continue to appear on behalf of the appellant on certain occasions particularly after the appellant had resumed personal conduct of the proceedings and was, in any event, represented by an advocate
katika sheria, Mtu huweza kuwasilishwa katika jambo lolote kwa kupitia njia mbali mbali, iliwemo kwa kutumia nyaraka maalum Nguvu ya kishiria, Power of Attorney (POA). POA huwa inaeleza mawanda ya kazi ya mpewa nguvu huyu, ambapo huwa ni nguvu ya kufanya kazi kiujumla katika jambo husika (General power of attorney) au nguvu ya kufanya kazi aina moja kama ilivyo bainishwa katika nguvu hiyo ya kisheria specific power of attorney.
ikumbukwe kama mtu alipewa nguvu ya kufanya jambo moja tu haruhusiwi kwenda nje na jambo hilo, na akienda anakuwa amefanya makosa kisheria ambapo huwa na madhara makubwa kisheria.
POA hufanya kazi hasa pale ambapo mtu anayetoa nguvu/ majukumu hayo hayupo na hawezi kabisa kufanya jambo hilo. ikitokea mtoa POA, hayupo, mpewa power akafanya kazi yake ... punde mtoa power (principal) akirudi na kujitambulisha na kuendelea kufanya majukumu yake mpewa power hawezi tena kuendelea kabisa na majumuku yake... na hiyo POA inakufa hapo, kama ataendelea chochote kitakacho endelea kitakuwa hakitambuliki kisheria.
maneno haya yalisemwa na kusisitizwa na mahakama ya rufani Tanzania katika shauri la Monyteri Pettit vs Jerome I. Shirima & Others (Civil Appeal No. 188 of 2023) [2026] TZCA 876 (7 August 2026), ambapo ilisema kimombo kama ifuatavyo.
"The Donee could no longer lawfully draft, sign or verify the amended Land Application or thereafter continue to appear on behalf of the appellant on certain occasions, particularly after the appellant had resumed personal conduct of the proceedings and was, in any event, represented by an advocate"